Featured

    Featured Posts

Loading...

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMUUA MKEWE KISA WIVU WA KIMAPENZI, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Mkazi wa Kijiji cha Ussonge, Kata ya Nyandekwa, Mkungu Kodoli (50) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora akikabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe.

Akimsomea mashtaka jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Ajali Milanzi, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Frank Matiku alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 26, mwaka huu saa 4.30 usiku nyumbani kwake.

Matiku alidai kuwa mshtakiwa alimpiga mkewe, Nsungurwa Dotto (46) kwa fimbo kichwani na kusababisha kifo chake.

Alidai chanzo cha mauaji hayo ni baada ya mshtakiwa kumfumania mkewe akifanya mapenzi na mwanaume mwingine. Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi za mauaji hadi atapofikishwa Mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika.

Matiku alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Milanzi kuiahirisha hadi Juni 14, itakapotajwa tena.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top