Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kutembelea barabara ya mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam huku akiagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale watakaokiuka kwa kufanya matumizi ya barabara za magari hayo kinyume na utaratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kimara mwisho mara baada ya kumaliza ziara hiyo ya kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka Waziri Mkuu amesema aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na pia kuona abiria wanaelewa vizuri namna ya kuitumia huduma hiyo.
Kwa nyakati tofauti wahudumu wa mradi huo pamoja na Mkurugenzi wa UDART wamemweleza Waziri Mkuu kuwa zipo changamoto mbalimbali ikiwemo matumizi ya tiketi zilizoisha muda wake pamoja na baadhi ya wananchi kutokuwa na uelewa wa mfumo unaotumika katika utoaji tiketi hizo pamoja na utekelezaji wa mradi huo.
Waziri Mkuu Mh Majaliwa ametoa onyo hilo kwa waendesha pikipiki, magari na watembea kwa miguu kuacha kukatiza hovyo na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuzuilika huku akitaka kikosi cha usalama barabarani kusimamia zoezi lautekelezaji agizo hilo hasa kwa wale wanaokuwa wakilala katika vivuko vya mabasi hayo hasa nyakati za usiku.
Katika hatua nyingine Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani amewataka wananchi kutii sheria bila shuruti ikiwa pamoja na kufuata taratibu zinazotakiwa katika matumizi ya barabara hizo pamoja na vivuko ili kuondoa usumbufu kwa watumiaji wengine, huku baadhi ya mashuhuda wa ziara hiyo wakipongeza hatua hiyo.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies