Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza harakati za kutafuta utaalamu wa uchimbaji wa mafuta na gesi ambapo wataalamu mbalimbali wa serikali wameanza kupatiwa taaluma hiyo kimataifa.
Akifungua mkutano maalum wa wadau wa sekta ya nishati ambao umeandaliwa kwa pamoja kati ya mamlaka ya usafiri baharini na serikali ya Norway kupitia taasisi yake ya uchimbaji wa mafuta baharini naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, mawasialino na usafirishaji wa Zanzibar Shomari Omar Shomari amesema sasa ni wakati muafaka kwa Zanzibar kujipanga kwa sekta hiyo kwa vile matarajio ya kupata nishati hizo zipo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri baharini Abdi Omar Maalim amesema mkutano huo utawawezesha wadau kupata mbinu za kujiandaa na athari za mafuta baharini huku baadhi ya washiriki wakiwemo wa sekta ya ulinzi wa bahari na uchimbani wa mafuta wamesema wameanza kupata mwelekeo wa hali ya nchi inapokabiliwa na ajali zozote za bahari zianzotokana na mafuta na gesi.
Wataalamu hao watatu wa Norway kwa siku mbili wanatarajiwa kutoa mwelekeo na mbinu za kupambana na uharibifu wa mazingira baharini unaotokana na uchimbaji wa mafuta na gesi na mikakati ya kupambana nayo.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies