Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza bajeti yake ya mwaka 2016 ambapo imepania kuongeza nguvu kwenye makusanyo ya kodi zilizokuwepo na kuwaahidi wafanyakazi wa kima cha chini wataanza kupata mshahara wa laki tatu kuanzia April mwakani.
Akisoma bajeti hiyo waziri wa fedha na mipango wa Zanzibar Dr Khalid Mohamed amesema hakuna kodi mpya itakayoanzishwa ila itaziendelea kodi kadhaa ambazo zipo lakini hazifanyiwi kazi huku akisema kuanzia mwaka ujao wa fedha malipo mengi ya kodi yataanza kuteklezwa ikiwa ni pamoja na malipo ya kodi za usafilishaji wa magari sasa yatafika Zanzibar na sio Tanzania bara,
huku pia serikali kuanzia sasa haitoruhusu gari kutokuwa na namba za usajili WZA Zanzibar na kuzirekebisha kodi kadha za ardhi, uuzaji wa nyumba miundombinu na kodi ambazo ziko lakini hazitumiki.
Kuhusu maslahi ya wafanyakzi waziri wa fedha Dr Khalid Mohamed amesema serikali tayri imekubali kuongeza kiwango cha chini cha mishahara kuanzia April mwakani na pia kupunguza kiwango cha kodi ya mshahara ya wafanyakazi kutoka asilimia 13 hadi tisa.
Waziri wa fedha pia amesisitiza nia ya serikali kuendeshwa kwa misingi ya utawala bora na kuhakikisha serikali inawatumikia wananchi kwa kuwawekea mazingira mazuri ya afya, elimu na miundombinu ya kisasa itaanza na mikakakati mpya wa kubana matumizi na kuhakikisha fedha zinatumika kwa maendeleo ya wananchi na kuzibana kodi za misamaha.
Bajeti hiyo ya Zanzibar kwa mwako ujao wa fedha inarajiwa kuwa ya shilingi biloini 841.5, ambapo bilioni 482.4 za mapato ya ndani, bilioni 324.8 kutokana na ruzuku na mikopo huku hadi sasa Zanzibar ina deni la taifa ni bilioni 398.6 na deni la nje 211.8 biloini.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies