Hatimaye Kamati ya Kudumu ya Hesabu Bunge za mashirika ya Umma-PAC- imeamua kuunda kamati ya wabunge tisa na kuipa mwezi mmoja kufanya uhakiki ripoti ya utekelezaji pamoja na mkataba uliongiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprise kutokana na kutoridhika na ripoti hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha kamati hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa PAC Mh.Aeshy Hilary amesema uamuzi wa kuundwa kamati hiyo umekuja kufuatia kutorishwa ripoti hiyo pamoja na kuwepo kwa changamoto katika taarifa ya utekelezaji wa mradi huo iliyowasilishwa na Jeshi la Polisi.
Aidha akizungumza majukumu ya kamati hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Mh.Josephat Asunga,mh.hilary amesema hiyo itaenda katika kila kituo ambacho Jeshi la Polisi linasema limefunga mitambo ya kuchukua alama za vidole na kufanya mahojiano na watu watakaoona wanaweza kupata taarifa za uhakika.