Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WAUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 AU FAINI YA TSH. BILLIONS 108.7, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imewahukumu raia wawili wa china kulipa faini  ya shilingi bilioni 108.7 ama kwenda jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kukutwa  na meno ya tembo  706.

Raia hao wawili wa china, XU FUJIE na HUANG GIN wanaotetewa na makili Edward  Chuwa na Nehemia Nkoko walihukumiwa kifungo hicho na Mh.Hakimu Mfawidhi,Cyprian Mkeha akisoma huku hiyo Mh.Mkeha amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi  tisa wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi wao na hivyo kuwakuta washatakiwa hao na makosa kadhaa.

Hakimu akaongeza kuwa  kwa kuzingatia hali halisi ya kesi,ushahidi na  hasara ambayo taifa imeipata kutokana na tembo 226 kupoteza maisha kwa kuuwa  ni wazai kuwa  raia haoa wa wachina wanatakiwa kupatiwa adhabu kama hiyo.

Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, hakimu Mkeha amesema ametoa adhabu hiyo pia kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa serikali,Faraja Nchimbi Paul  Kadushi na Wankyo Simon na maombi ya utetezi  kuwa wapunguziwe adhabu.

Awali kabala ya huku hiyo mawakili wa serikali,nchimbi aliiomba mahaka iwape adhabu kali washtakiwa hao kwa kuwa kati ya kipindi cha 2010 na  desemba 2013  hapa chini jumla ya tembo 892 waliuawa .

Alidai kuwa washtakiwa hao waliingia nchini 2010 hadi novemba 2013 walipokamatwa kwa makosa hayo na kuwepo  rumande  matukio ya mauaji ya tembo yalipungua.

Nchimbi alibainisha kuwa washtakiwa hao waliiua robo ya tembo wanaouawa hapa nchini na kwamba kutokana na wingi wa nyara walizokutwa nazo inaonekana wazi ni miongoni mwa vinara wakubwa , wawezeshaji na wahusika wa shughuli za  ujangili zinaeoendelea hapa nchini.

Novemba 2, 2013 katika mtaa wa kifaru mikocheni kinondoni washtakiwa hao wanadaiwa kukamatwa wakiwa na nyara hizo za serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 1,880 na thamani ya sh 5,435,865,000 wakivimiliki bila ya kuwa na  kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.


Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top