Featured

    Featured Posts

Loading...

WAWEKA KAMBI MBUGANI KWA SIKU 12 WAKIKESHA, BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Wakulima na Wafugaji wa jamii ya Wadatoga waweka kambi mbugani kwa siku 12 wakikesha.

Kundi la wakulima na wafugaji wa jamii ya wadatoga idadi kubwa wakiwa wanawake wa jamii hiyo ya wafugaji zaidi ya 200 wameweka kambi na kulala katika mbuga ya bonde la Zimbabwe wilayani Babati mkoani Manyara kwa takribani siku 12 sasa wakidai kulalamikia unyanyasaji unaofanywa na askari wa jumuiya ya hifadhi ya jamii (JUHIBU) dhidi yao pamoja na kutozwa tozo la mamilioni ya fedha za mifugo inayokamatwa askari hao.

Wakizungumza na Mutalemwa Blog  makundi hayo ambayo tayari wameshajenga vyoo na mahema katika eneo hilo la kijiji cha Kazaroho huku muda mwingi wakiimba nyimbo mbalimbali wametaja sababu tatu za kuweka kambi hiyo ikiwa ni pamoja na kupigwa, kutozwa faini ya mifugo isiyokuwa na stakabadhi za halmashauri, kuwekwa mahabusu za vijiji pamoja na kutakiwa kuondoka katika eneo hilo ambalo wanao uhalali lakini mamlaka husika za ngazi ya wilaya ya mkoa zimeshindwa kutatua mgogoro huo.

Nae kamanda wa polisi mkoani Manyara Bw Camillius Wambura amesema kwa upande wa polisi haijapokea malalamiko yeyote ya mwananchi aliyenyanyaswa na kudai polisi imefanya uchunguzi wa kina juu ya madai hayo dhidi ya askari wa jumuiya hiyo yajamii(JUHIBU) na wametoa nafasi kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ifanye kwanza kazi yake.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama DC Crispin Meela amekiri kuwepo kwa kambi hiyo na kudai chanzo chake si unyanyasaji bali kutafuta njia ya kupinga agizo la kutakiwa kuondoka katika eneo hilo ambalo limebadilishwa matumizi kuwa maeneo ya hifadhi ya taifa,lakini kulingana na mkusanyiko huo serikali itatumia nguvu kuwaondoa endapo watagoma kuondoka wenyewe.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top