Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WANAFUNZI 12% WATELEKEZWA NA WAZAZI MKINGA, BOFYA HAPA KUJUA CHANZO CHAKE

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Asilimia 12% ya wanafunzi watelekezwa na wazazi Mkinga

Serikali imeombwa kuingilia kati kufuatia asilimia 12% ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani Mkinga Kutelekezwa na wazazi wao waliokimbilia mijini kisha kuwaacha watoto wao walelewe na bibi zao ambao baadhi yao hawana mwamko wa kieleimu hatua ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kuacha shule kwa sababu ya kukosa mahitaji muhimu ikiwemo sare za shule,vitabu na vyakula.

Wakizungumza katika shule ya msingi boma iliyopo kata ya boma wilayani Mkinga wakati wasamaria wema kutoka taifa la marekani walipokuwa wakiwakabidhi baadhi ya wanafunzi hao msaada wa vifaa mbali mbali vya elimu ili kuwapunguzia makali ya maisha,baadhi ya walezi na walimu wa watoto hao wameiomba serikali kudhibiti  tatizo hilo kwa sababu baadhi ya wanafunzi wameamua kusitisha masomo yao kisha kwenda kujikita katika shughuli za kujipatia kipato ikiwemo uvuvi huku wengine wa kike wakipewa ujauzito.

Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Mkinga Bibi Mboni Mgaza amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuziagiza mamlaka husika kuwafuatilia wazazi wanaotuhumiwa kuwatelekeza watoto ili wahakikishe wanasimamia elimu kwa watoto wao badala ya kuwaachia kazi hiyo wazee ambao wanaohitaji kusaidiwa.

Kufuatia hatua hiyo msamaria mwema Iloyd Jameson kutoka taifa la marekani aliyeguswa na tatizo hilo amesema ni wajibu kwa wanafunzi wapatiwe vitendea kazi vya shule ili waweze kuwa na mwamko wa kielimu kisha kuahidi kuwawekea nishati ya umeme wa mionzi ya jua katika shule ya msingi boma ili wanafunzi waweze kusoma kwa tija

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top