Wahamiaji haramu 15 wakamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba Singida.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi idara ya uhamiaji mkoa wa Singida imewakamata wahamiaji haramu kumi na tano waliokuwa wakitoka nchini Ephiopia na kuelekea Afrika Kusini na kufanya jumla ya wahamiaji thelasini kukamatwa mkoani Singida kwa kipindi cha kuanzia mwezi desemba mwaka Jana hadi Januari Mwaka huu.
Akieleza afisa uhamiaji mkoa wa Singida DCI Faith Ihano amesema wahamiaji hao haramu wamekamatwa na askari wa uhamiaji wakiwa katika doria wamekutwa wamehifadhiwa katika nyumba moja eneo la unyakindi manispaa ya Singida wakisubiri kusafirishwa kwenda Afrika Kusini.
Katika hatua nyingine DIC Ihano amesema wahamiaji hao haramu kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakisaidiwa na baadhi ya watanzania wana ofanya biashara haramu ya kuwasaidia kupita nchini kwa njia ambazo siyo za halali na atakaye bainika hatua kali za kisheria zita chukuliwa dhidi yake ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.
Wakihojiwa na Mutalemwa Blog wahamiaji hao haramu ambao wote hawajui kuongea kiswahili wala kingereza isipo kuwa mmoja wao Bwana.Mohamed Ndermon anaye ongea kingereza kwa shida ,wamesema walikuwa wkienda Afrika Kusini wakitokea nchini Kenya kwa kutumia usafiri wa gari dogo kwenda kutafuta maisha.
Kuhusiana natukio hilo idara ya uhamiajia mkoni Singida ina mshikilia mmiliki wa nyumba abayo wahamiaji hao haramu walikuwa wamehifdhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.