Featured

    Featured Posts

Loading...

POLISI WAKABILIANA NA WAVAMIZI KWENYE KITUO CHA POLISI, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Polisi wakabiliana na wavamizi kwenye kituo cha polisi Duthumi wilaya ya Morogoro.

Jeshila polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi zaidi ya 30 waliovamia kituo cha polisi duthumi kata ya Bwakila chini wilayani Morogoro waliokuwa na silaha za jadi, ambao wamevunja mlango mkubwa wa kituo hicho kwa nia ya kuwakomboa wenzao watatu,waliokuwa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na wizi wa mifugo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Grifton Mushi, amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kwamba wanawashikilia watu watatu zaidi kuhusiana na tukio hilo ambapo amedai kundi hilo la wananchi wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mashoka,mapanga na marungu,walivamia kituo hicho cha polisi Duthumi kwa nia ya kuwakomboa wenzao  waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mifugo ya  teu saningo,mkazi wa Bwakila chini,ambapo hata hivyo tayari watuhumiwa hao walikuwa wameshahamishwa.

Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zimedai kuwa awali wananchi walikuwa wameikamata mifugo hiyo wakituhumu kula mazao kwenye mashamba lakini  wakati wakiilinda walimchinja mmoja na  kumla, jambo lililofanya polisi kuwakamata waliohusika,ndipo kiongozi mmoja wa kisiasa akadaiwa kuwakusanya wananchi na kuwahimiza wakawakomboe wenzao,ndipo zilipozuka vurugu hizo.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo akizungumza kwa njia ya simu kutoka duthumi,ameeleza kushangazwa na hatua ya polisi kuachana na kesi ya msingi ya mifugo kula mazao,badala yake kuigeuza kuwa ya wizi wa mifugo,huku mfugaji aliyelisha mazao mashambani akiachwa huru,na kwamba katika  kuwatawanya,polisi wametumia silaha za moto zilizojeruhi baadhi ya watu waliokwenda kuwawekea dhamana wenzao.

Katika tukio jingine,wananchi wa kitongoji cha mizizini, kijiji cha Maseyu, wamechoma mabanda manne na vifaa vya uchimbaji madini, mali ya ayubu bishangazi, na kumjeruhi mwekezaji huyo , wakimtuhumu kutumia kemikali za sumu kusafisha madini,ambapo polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusika na tukio hilo.

Baadhi ya wananchi wa morogoro wamelaani kitendo cha baadhi ya watu wanaojichukulia sheria mikononi,pindi wanapotafuta haki,ingawa wengine wakadai kitendo cha kukamatwa kwa watuhumiwa na kuachiwa au kutochukuliwa hatua kimewafanya wananchi kukosa imani na serikali yao  hususani vyombo vya dola na kuamua kujichukulia sheria mikononi.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top