Featured

    Featured Posts

Loading...

OPERESHENI YA UTUMBUAJI MAJIPU KWA WASIO LIPA KODI HAINA NIA YA KUWAADHIBU WATU, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Majaliwa:Operesheni ya utumbuaji majipu kwa wasio lipa kodi haina nia ya kuwaadhibu watu.

Waziri Mkuu Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA amesema oparesheni ambayo inafanyika sasa kuhakikisha kila mtu analipa kodi na kudumisha nidhamu kwa watumishi wa umma haina nia ya kuwaadhibu watu.

Amesema hatua hiyo ni kuhakikisha kila mtu anatekeleza wajibu wake wa kulipa kodi ili serikali iweze kutekeleza mipango yake iliyojiwekea na hivyo amewaomba wananchi kuisaidia serikali kutekeleza oparesheni hiyo.

Mheshimiwa MAJALIWA ameyasema hayo katika mkutano wa Jumuiya ya Wanarukwa na Katavi waishio jijini Dar es Salaam ambapo amesema serikali haitamuonea mtu wala huruma mtu yoyote ambaye anakwenda kinyume na sheria za nchi.

Aidha mkuu huyo amewataka Watanzania kutumia fursa zinazowazunguka kama madini, kilimo, mifugo na nyingine za kujiletea maendeleo. 

Naye Waziri Mkuu Mstahafu MIZENGO PINDA amesema kwa sasa kila mtu anapaswa kujua kuwa ni jukumu lake kujiletea maendeleo kwani haitakuwa na faida yoyote kama mtu amebaki kuikosoa serikali bila ya kutoa njia mbayala ya kurekebisha hicho ambacho anaona hakijawa sawa.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top