Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MAKAZI KWENYE ENEO LA MASHAMBA YA MPUNGA IRINGA YAPIGWA MARUFUKU, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Serikali yapiga marufuku makazi kwenye eneo la mashamba ya mpunga Pawaga Iringa.

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi George Simbachawene ameuagiza uongozi wa mkoa wa Iringa kuwatafutia maeneo ya makazi ya kudumu waathirika wa mafuriko wanaoendelea kuokolewa kwenye mafuriko katika mashamba ya mpunga Pawaga ili kuhakikisha hakuna mtu anayerudi kuweka makazi ya kudumu katika maeneo hayo ili eneo hilo libakie la mashamba pekee.

Waziri Simbachawene amesema hayo alipowatembelea waathirika wa mafuriko waliookolewa kutoka kwenye mashamba ya mpunga Pawaga walikokuwa wamezungukwa na maji na kusema kuwa kuanzia sasa serikali inapiga marufuku vibanda vya muda pamoja na nyumba za kudumu kwenye mashamba hayo ili kuepusha kujirudia kwa janga hilo.

Akitoa taarifa ya zoezi la uokoaji kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa Bibi Lucy Nyalu amesema mpaka sasa watu walio kwenye kambi za muda wamefikia 419 ambapo idadi hiyo imepungua kutokana na baadhi yao kuchukuliwa na ndugu zao ama kuondoka makwao.

Waziri Simbachawene ameupongeza uongozi wa mkoa wa Iringa kwa juhudi za uokoaji zinazoendelea hadi sasa kukiwa hakuna kifo hata kimoja kilichokwisharipotiwa licha ya changamoto za ukosefu wa vifaa vya uokoaji na kuwaomba wadau mbalimbali kushirikiana na serikali kusaidia waathirika hao kwa hali na mali ambapo mkuu wa mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza amewataka waathirika hao kudumisha usafi ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Mapema kabla ya ziara ya waziri George Simbachawene shirika la afya duniani WHO limekabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo dawa za kusafisha maji zenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa lengo la kusaidia kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye kambi hizo za waathirika wa mafuriko huku waziri Simbachawene akikabidhi shilingi mil.5 zilizochangwa na watumishi wa ofisi yake.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top