Napenda niwahakikishie wazee na watanzania kwa ujumla, hatutawaangusha. Kwa niaba ya viongozi wenzangu, nawaahidi tutawanyia kazi, ninachowaomba wzee na watanzania kwa ujumla, mtuamini.
Katika shughuli zozote za kufanya mabadiliko huwa kuna changamoto zake, watakaoguswa ni wachache sana kwa ajili ya watanzania wote hasa maskini.
Haipaswi kuwa maskini, Tanzania hii ina utajiri wa kila aina, haipaswi kuwa na wanafunzi wanaokaa chini, watu wanaolala chini mahospitalini.
Lakini ni lazima tujue wapo watu wachache waliotufikisha hapa, mlituchagua kwa mioyo yenu wote, ndio maana nasema kwa dhati naomba mtuamini kwa sababu tunaamini tukiyatekeleza haya, nchi hii itakuwa ya mfano Afrika kama si duniani kwa ujumla.
Mimi na serikali yangu tumejitoa sadaka kwa ajili ya watanzania, tunaomba muendelee kutupa nguvu ili haya matamanio yetu kwa ajili ya Tanzania yoyote tena kwa hara.
Yoyote atakaejaribu kutukwamisha serikalini tutambomoa kwa ajili ya watanzania.
Wapo watu kwao pesa si tatizo na angalau wangezipata kihalali, lakini ni za wananchi wenye hali mbaya sana Kilometa moja imejengwa kwa bilioni mbili tena ni barabara ya halmashauri, nimekaa serikalini miaka 20 na sijawahi kutengeneza barabara kuu, kilometa moja kwa bilioni mbili lakini barabara ya halmashauri tena ya Bariadi inatengenezwa kwa mabilioni ya shilingi zilizokuwa zinatoisha kutengeneza zaidi ya kilomita 20
Waziri alienda kuangalia mafuta, PUMA na ORLX serikali ina share ya asilimia 50. Flow meter ambayo ndio inapima mafuta kiasi gani yanaingia nchini hakifanyi kazi miaka mitano na Dar es Salaam kila kona sheli.
Nilikutana na wakina mama wakaniambia twende ukaone, nilishaenda lakini ilikuwa upande mwingine, wasaidizi wangu wakaniambia usiende lakini nikaenda.
Nikakuta maji ya kutoka chooni yanaingia, wakina mama wamelala chini wakati kuna jengo linajengwa tangu awamu ya mzee Mwinyi halijaisha mpaka leo.
Wazee tunapochukua hatua, sisi si wakatili sana, tunawawakisha nyinyi uchungu wenu. Ninafahamu mawaziri wangu wanafanya kazi nzuri. Ninawapa muda na nyinyi muwape muda na mimi mnipe muda.
Lile jengo linalotumika kama ofisi ya uzazi wa mpango wahame na waziri atajua atawapeleka wapi tena ofisi kama ya waziri, anaweza kwenda kukaa nao ofosini kwake, wale kina mama waliokuwa wanalala chini wahamie hapo.
Ninawaomba katika kipindi hiki cha mpito mtuvumilie, majipu tutayambua kweli kweli.
Tanzania haiwezi kwenda mbele bila kuwa na fedha zake, wafanyabiashara wanakwepa sana kodi. Tunataka fedha tunazozikusanya ziende kuwasaidia watanzania wa hali ya chini.
Zipo kejeli nyingi kuwa ni nguvu ya soda, hata kama ni soda ukiweka gongo utalewa, kwa hio hii ni soda special.
Tumeweka bilioni 200 kwa ajili ya daraja la Coco beach hadi Agha Khan, barabara ya kutoka Rangi tatu pia tumeitengea fedha na interchange ya ghorofa tatu pale Ubungo.
Shirika la ndege tunataka kulifufua ndio maana tunachukua hatua mbalimbali. Yuko mmoja ameshikwa pale alikuwa anataka kubadilisha fedha kwenye akaunti tukamkamata, hatutaki kusema mengi kwa sababu hatua zinachukuliwa ikiwemo za kimahakama.