Ndugu mwana jamii wa mtandao wa Mutalemwa Blog, hapa nimekuwekea matukio kadhaa yaliyojili siku ya leo, na kwakuanza tuna anzia huko makao makuu ya nchi mkoani Dodoma ambapo
1. Mhe.Job Ndugai amechaguliwa kuwa spika wa bunge la kumi na moja 11
2. Huku nchi ya Uingereza yakubali kusaini mkataba wa kusaidia shule 12 za Tanzania ikiwa ni harakati za kuboresha elimu nchini.
3. Mgonjwa aliyegundulika kuwa na Ebola nchini Guinea aruhusiwa baada ya kutibiwa hadi kupona.
4. Tume ya uchaguzi nchini Tanzania yavitaka vyama vya Siasa vilivyoshindwa katika uchaguzi mkuu vikubali matokeo.
5. Mbali ya kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la kumi na moja 11 Ndugai amewaapisha wabunge wateule wa bunge la kumi na moja 11.
6. Nauko mkoani Kigoma mhe.David Kafulila afungua shauri mahakama kuu kanda ya Tabora kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Kigoma kusini.
7. Wazazi watakiwa kuwasaidia watoto wa kike ili kuwakinga na mimba katika umri mdogo.
8. Urusi yathibitisha kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege yake nchini Misri kilitokana na milipuko ya mabomu.
9. Sekta ya maziwa nchini yashindwa kulinufaisha taifa kutokana na uchache wa Ng'ombe wa maziwa tulionao.
10. Vodacom tanzania yatumia zaidi ya Trilioni 2 katika uwekezaji wake hapa nchini.
11. Kwa upande wa michezo, timu ya taifa ya Tennis ya walemavu yakabiliwa na ukosefu wa vifaa maalum vya michezo
12. Na mechi kati ya Ufaransa na Ubeligiji yaahirishwa kutokana na hofu ya usalama