Watu 700 waliokuwa wamejiunga na
makundi ya wapiganaji Somalia wametoroka na kurejea Kenya, ripoti ya
Shirika la Kimataifa kuhusu Uhamiaji (IOM) inasema.
Ripoti hiyo inaonya kuwa ni hatari kukosa kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida katika jamii.
Kundi
la wapiganaji wa Kiislamu la al-Shabab katika taifa jirani la Somalia
limekuwa likisajili watu kutoka eneo la kaskazini mashariki la Kenya.
Kenya imeshuhudia msururu wa mashambulio kutoka kwa wapiganaji hao.
Mapema mwaka huu watu 148 waliuawa baada la wapiganaji wa kundi hilo kushambulia chuo kikuu cha Garissa.
Ingawa
ripoti hiyo haijataja watu hao waliorejea Kenya walitoka kwenye makundi
yapi, Naibu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya (Supkem) Hassan
Ole Nadu amethibitisha kwamba walikuwa wamejiunga na al-Shabab.
Ripoti hiyo ya kurasa 36 ilitayarishwa na IOM, Supkem na wizara ya masuala ya ndani nchini Kenya.
Watafiti
waliohusika kuandika ripoti hiyo waligundua kuwa wengi wa watu wazima
waliojiunga na wapiganaji hao walifanya hivyo kwa hiari.
Thuluthi ya watoto waliokuwa wamejiunga na makundi hayo walishurutishwa.
Kurejea kwa vijana hao kunatoa “fursa na pia hatari kwa Wakenya.”
“Kwa
upande mmoja wanaweza kutumiwa kukabiliana na mafunzo ya kueneza
itikadi kali na pia juhudi za makundi hayo kupata wafuasi, ripoti hiyo
inasema.
"Kwa upande mwingine, hatua wanazochukua maafisa wa
usalama zinaonekana kuwafanya watu kuzidi kuwa na misimamo mikali kwani
wanaorejea wanajihisi kuwa hatarini. Hawana njia bora ya kurudi tena
katika jamii.”
Walioshiriki katika utafiti huo walitaja usalama
kama jambo linalowazuia zaidi katika juhudi zao za kurejelea maisha ya
kawaida katika jamii.
Jumla ya watu 185 walihojiwa, ambao ni karibu 30% ya watu 684 waliorejea Kenya baada ya kuondoka makundi hayo ya wapiganaji.
Wengi walikuwa na umri wa kati ya miaka 18 na 34.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies