Mgombea urais kupitia chama cha ukombozi wa uma– CHAUMA Hashim Rungwe
amesema, akichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu ujao, atahakikisha
kilimo cha umwagiliaji kitafanywa na helkopta na ndege, ili kuongeza
uzalishaji wa mazao katika kukabiliana na tishio la njaa nchini.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya mkuti wilaya ya
Masasi mkoani Mtwara, Mheshimiwa Rungwe amesema, inasikitisha kuona
taifa baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhuru, wananchi wake wamekuwa
wakikabiliwa mara kwa mara na njaa kutokana na kilimo cha kutegemea
mvua, huku nchi ikiwa na mabonde mengi mazuri kwa kilimo, na hivyo
akasisitiza, akichaguliwa kuwa rais wa serikali ya awamu ya 5,
atahakikisha kilimo cha umwagiliaji kitafanywa na helkopta na ndege, ili
taifa lijitosheleze kwa chakula.
Aidha kwenye mkutano huo, Mheshimiwa Rungwe aliwauliza wananchi
kama watamchagua kuwa rais wao, nao walimwitikia kuwa watamchagua,
ambapo alidai yeye anafaa kuchaguliwa kuwa rais, kwa kuwa sio mwizi au
fisadi, na kuongeza, moja kazi atakayofanya akichaguliwa, ni kuimarisha
kitengo cha uanasheria, ili wananchi wenye matatizo ya kisheria, waweze
kusaidiwa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies