Polisi nchini Ujerumani wameonya wazazi dhidi ya kuweka picha za watoto wao hadharani katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
Katika
ujumbe kwenye ukurasa wao wa Facebook, polisi wa eneo la Hagen
wametahadharisha wazazi kuwa picha hizo zinaweza kunakiliwa au
kubadilishwa na kutumiwa vibaya na watu wanaovutiwa kimapenzi na watoto.
Aidha, watoto wahusika huenda wasipendezwe na picha hizo kuwa wazi mitandaoni watakapokomaa na kuwa watu wazima.
Wazazi wameshauriwa kuhakikisha kuwa picha hizo, ikilazimu, zinatazamwa na marafiki zao pekee na si kila mtu mtandaoni. Ushauri huo wa polisi hao umeenezwa sana mtandaoni na kuvutia hisia mseto.
Afisa msemaji wa Polisi wa Hagen ameiambia BBC kwamba walishangazwa na jinsi ujumbe huo wa tahadhari ulivyopokelewa.
Amesema wanakadiria kuwa umesomwa na watu zaidi ya milioni 12.
"Tunataka
kuwaambia watumiaji wote wa mitandao ya kijamii kwamba ni muhimu kuwa
makini na kila kitu wanafanya kwenye mtandao," amesema Hanki Ulrich .
"Ni bora kufikiria mara mbili - mtandao hausahau kamwe "
Bw
Hanki ameongeza kuwa ujumbe huo haujaongozwa na matukio yoyote mapya ya
kesi za uhalifu au watu wanaovutiwa na watoto kimapenzi huko Hagen.
Picha zilizobadilishwa
Shirika
la kujitolea linalohusika na ulinzi wa watoto NSPCC katika taarifa yao
wamesema: " Wazazi wote wanapaswa kujisikia huru na kufurahia kuchukua
picha za watoto wao na kushirikiana nao na marafiki na familia. Hata
hivyo, tunapaswa wote kuwa makini wakati wa kuziweka picha hizo
mitandaoni.
"Tunajua kwamba wahalifu wa ngono wana uwezo wa
kubadilisha picha za watu wasiokuwa na hatia, na maendeleo katika
programu za kuhariri picha zimefanya hili kuwa rahisi sana.
"
Hivyo kama wazazi watachapisha picha za watoto wao kwenye mitandao,
wanapaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba wanachunguza hali yao ya
faragha na kuhakikisha wanaridhishwa na watu watakaotazama picha hizo."
Shirika
hilo limeongeza kuwa iwapo wazazi wana wasiwasi kuwa picha ya mtoto wao
imeanguka mikononi mwa watu wabaya, wanapaswa kuwasiliana na Internet
Watch Foundation, Child Exploitation na Online Protection Centre (Ceop)
au kuwasililiana na NSPCC kupitia numbari ya msaada ya simu ya 0808 800
5000 ambapo watapokeza usaidizi.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies