Muda mfupi uliopita, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim
Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema
kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka
vituoni, yeye amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa
CCM
anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein, na kuitaka Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye
fomu zinazotoka vituoni. Mengi zaidi, sikiliza matangazo yetu ya leo
mchana.
Source:DW (Kiswahili)
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies