Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ZITTO KABWE NDANI YA UWANJA WA TAIFA JUMA MOSI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

WAKATI kiongozi wa Chama cha ACT Wazendo, Zitto Kabwe, ameomba Watanzania waruhusiwe kuingia bure uwanjani kuishangilia Taifa Stars dhidi ya Nigeria keshokutwa Jumamosi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vikubwa kwa ajili ya mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017.

Wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kuhusu uchaguzi mkuu mwaka huu zilizofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam Jumapili, Zitto alishauri TFF iruhusu mashabiki waingie bure kwenye Uwanja wa Taifa kuipa sapoti kubwa timu ya nyumbani.

Hata hivyo, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo, Baraka Kizuguto, ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, ametangaza kiingilio cha chini ya Sh 7,000 huku akimjibu kwa kifupi Zitto kwa kusema: “Tusichanganye siasa na michezo”.

Kizuguto amesema maandalizi ya mechi hiyo ya Kundi G yamekamilika huku akieleza kuwa kiingilio cha juu (VIP A) Sh 40,000, VIP B Sh 30,000, VIP C Sh15,000, Rangi ya Machungwa Sh 10,000 wakati viti vya rangi ya Bluu na Kijani Sh 7,000. 

Amesema tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo saa 4 asubuhi katika vituo 10; Ofisi za TFF, Buguruni, Mbagala, Ubungo, Makumbusho, Uwanja wa Taifa, Mwenge, Kivukoni, Posta (Luther House) na Kariakoo (Msimbazi). 

Amesema mechi hiyo itakayoanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili jijini leo jioni.

Marefa hao ni Louis Hakizimana (kati), Honore Simba (msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (msaidizi) na Abdoul Karim Twagiramukiza (wa akiba) pamoja na kamisaaa Charles Kasembe kutoka Uganda.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top