Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mwaka 2012 kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alikuwa wa kwanza kuomba kumsajili mtoto wa Lionel Messi ili akikua ajiunge na Academy ya Arsenal, hiyo inaonesha pia kwamba kuna watoto wengi wa wanasoka hupewa nafasi kubwa ya kufuata nyayo za baba zao.
Nimekusogezea picha na video za watoto wa mastaa waliofuata nyayo za baba zao.
1. Enzo Zidane ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Real Madrdid ya Hispania Zinedine Zidane... Enzo amefuata nyayo za baba yake na hivi sasa yupo katika timu ya vijana ya Real Madrid. Enzo ni mjanja na anajua kuuchezea vizuri mpira kama baba yake.
Enzo na baba yake Zidane
2. Rivaldinho ni mtoto wa Rivaldo staa wa soka kutokea Brazil lakini pia amewahi kuichezea FC Barcelona ya Hispania kwa mafanikio, Rivaldinho amefuata nyayo za baba yake kwa kuanza kuichezea klabu iliyomlea baba ya Mogi Mirim na kwa sasa wanacheza pamoja na baba yake katika klabu hiyo.
Rivaldo na mtoto wake Rivaldinho
3. Tom Ince ni mtoto wa staa wa zamani wa Uingereza Paul Ince ambae amewahi kutamba katika vilabu vya West Ham United, Manchester United na Liverpool ila Tom anachangamoto kubwa ya kupata mafanikio kama aliyofikia baba yake. Tom Ince kwa sasa anaichezea Derby County.
Paul Ince na mtoto wake Tom
4. Justin Kluivert yupo katika Academy ya Ajax Uholanzi baba yake Patrick Kluivert amewahi kutamba katika klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.
Justin Kluivert na baba yake Patrick Kluivert
5. Joe van der Sar ni mtoto wa golikipa wa zamani wa Manchester United Edwin van der Sar, amefuata nyayo za baba yake si kwa kucheza soka tu bali hata nafasi anayoichezea ni sawa na baba yake. Joe yupo katika Academy ya Ajax.
Joe na baba yake Edwin van der sar
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.