Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SABABU YA DK.SLAA KUJIUZULU NI MKE WAKE? SOMA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Wakati uvumi wa kujiuzulu cheo na kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),  Dk. Wilbroad Slaa, ukiwa umetawala kupitia mitandao ya kijamii na magazeti, taarifa zinadai kuwa sababu ya kuchukua hatua hiyo ni shinikizo kutoka kwa mkewe.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti moja likimnukuu Dk. Slaa mwenyewe, zilisema ameachana na siasa na kujivua wadhifa wake na atabaki kufanya shughuli zingine.

Dk. Slaa  amedaiwa hakubaliani na namna chama chake kilivyompokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.
Lowassa aliyekuwa Mbunge wa Monduli alitangaza kuhamia Chadema, Julai 28, mwaka huu  baada ya kutoridhishwa na mchakato wa CCM wa kumpata mgombea wa urais.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya Chadema zinadai, Dk. Slaa alishiriki katika mchakato mzima wa kumpokea na kuridhia Lowassa, kusimamishwa kuwa mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Hata hivyo, chanzo kingine cha habari kinadai kuwa mke wa Dk. Slaa, Josephine Mashumbusi, alitoa shinikizo kwa mumewe la kujiuzulu baada ya kuruhusu kusimamishwa mgombea mwingine (Lowassa).

“Josephine alikuwa na uhakika mume wake ndiye atakayesimama ugombea urais kwa upande wa Ukawa, hali ilivyobadilika, akakasirika na kumwambia mumewe ama yeye au Chadema,” chanzo kilidokeza.

Kupitia ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, unaoonyesha kutoka kwa Mashumbusi, aliandika “Ni kweli Frida na kwa hili Dk. Slaa amejivua wadhifa wake wa ukatibu mkuu na kuachana na siasa.

Hata hivyo, Dk. Slaa alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kuthibitisha madai hayo, iliita mara moja na kuzimwa. Juhudi za kumpata ziligonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana hali kadhalika simu ya Mashumbusi.

Baadhi ya wasomi walisema kama Dk. Slaa amejiuzulu nafasi yake  na kujivua unachama atakuwa amejijengea heshima na uaminifu na kwamba Chadema kitapata pigo.

Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema  kwa upande wake aliamini kitu kama hicho kitatokea kutokana na tukio hilo kuwa la haraka na kulifananisha sawa na mapinduzi ya ghafla ndani ya chama.

Mhadhiri huyo alisema anaamini Slaa aliweza kukifufua chama hicho mwaka 2010 kwa kuweka misingi yake ya kukemea ufisadi, hivyo hawezi kurudi nyuma kwa kuivunja.

Dk. Kitlya Mkumbo kwa upande wake alisema anaheshimu maamuzi ya pande zote mbili kwani zinaonyesha demokrasia na ukomavu wa kisisa.
Septemba 15 mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa alimtaja Lowassa kuwa miongoni mwa mafisadi 11 waliochota fedha Benki kuu katika akaunti ya Epa.

Kauli hiyo alikuwa akiitamka kila mahali alipokwenda na  kusisitiza kwamba Lowassa na viongozi wenzake wa CCM wamechafuka kwa ufisadi.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top