Mbunge
wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama
ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa
jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa
Singida.
Singida
MBUNGE
wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji
amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa
miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.
Mbunge
huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika
uwanja wa People's Club (MB) wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa
Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu
wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.
Miradi
hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za sekondari kutoka mbili
hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya na kupeleka shule watu wenye
mazingira magumu elfu 15.
Alisema
ametekeleza majukumu yake ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake la
uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati
huo ikiwamo elimu na Afya
Alisema
kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni kunatokana na majukumu
ya biashara zake kuwa makubwa pamoja na kutaka kuwa karibu na familia
yake baada ya miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia
kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha wakati wa awamo ya kwanza,
nafikiri ni busara sasa kutimiza majukumu haya ya familia ambayo
niliyabania nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia
siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu yamebadilika katika kipindi
cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji wa biashara zangu umeambatana na
kuongezeka kwa majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo
huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana kwa sababu mafanikio
yangu kwenye biashara ndiyo yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na
yatakayo-niwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa
vitendo." alisema.
Akizungumzia
sekta ya afya alisema wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana
vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya
vyandarua 6000 kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa
kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini
ya miaka 5 kwa asilimia hamsini" alisema akishangiliwa.
Aidha
alishirikiana na mamlaka husika kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa
jicho kwa kupeleka madaktari bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya
mkoa, waliotoa huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya
wananchi 1,000.
"Tulifanikiwa
kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa
kuchangia ujenzi, wa zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo
zimekamilika! na zahanati ya kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi
unaendelea." alisema
Pamoja
na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu
na kufunga solar panel, pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye
zahanati za Manga na Unyambwa!
Akifafanua
zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba walijenga vyumba vya
madarasa, kuweka matangi ya maji ya kuvunia maji ya mvua, vyoo, na
kusambaza madawati katika shule mbali mbali za msingi na sekondari
jimboni Singida mjini.
Aidha
alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule
zetu zote, za serikali ndani ya manispaa, ya Singida na tulifanikiwa,
kuwapeleka wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya
kujifunza bungeni.
Akizungumzia
sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa
Suwasa na vingine 45 ndani ya baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya
Singida.
Aidha
alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10, unaofadhiliwa na benki
ya dunia, akisisitiza kuwa wakati akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa
maji safi na salama ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji
umefikia asilimia 81.
Pia
alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga barabara za kiwango,
cha changarawe ndani ya manispaa na kufanya manispaa kuwe na barabara
zinazopitika kwa kipindi chote!
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza kutogombea tena.
Akiwashukuru
wananchi wa Singida alisema kwamba: "kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu
kubwa sana niliyo-barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na
najisikia kuwa nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu
Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake, ikiwemo mimi
mwenyewe."
Alisema
dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama
mwanasiasa, akisisitiza kuwa dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na
mapenzi aliyonayo kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga
Singida.
"Mapenzi
yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo
kuwa, haya yatajitokeza katika njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.
"Naomba
nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na kada wa CCM,
mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge katika shughuli zote za
maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi,
kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na
mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! "
Mwanamama
huyu akiwa haamini macho yake huku machozi yakimlenga lenga baada ya
kusikia Mbunge wake kutogombea tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.
Watoto
hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada ya kumsikia mbunge
wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la ubunge wa Singida mjini.
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
Mbunge
wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji
cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni mlemavu wa macho na miguu
aliyefahamika kwa jina moja tu la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano
wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya
ubunge wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea
tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya People's Club.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa Singida mjini.
Mwanamuziki
wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akitumbuiza wananchi wa Singida
mjini wakati wa mkutano mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani
ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa
jimbo hilo.
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake wakishambulia jukwaa.
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya Diamond Platnumz.
Diamond
Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake wakitia mbwembwe kwenye
show ya kukata na shoka katika viwanja vya People's Club, Singida mjini.
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
Umati
wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika katika viwanja vya
People's Club kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa
miaka 10 ya ubunge wa Mh. Mohammed Dewji.
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa wananchi wa Singida mjini.
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
Kijisehemu
cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini waliojitokeza katika mkutano
uliotishwa na Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia) akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses Iyobo.
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.