Leonard
Derefa( Mwanaderefa) alizaliwa mwaka 1942 katika kijiji cha Bulima wilaya ya Misungwi mkoani
Mwanza na hadi umauti unamfika alikuwa anaishi katika mtaa wa Mbuyuni kata ya
Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Mmoja wa watoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Newe Derefa amesema
baba yake alifikwa na umauti leo asubuhi saa 12.30 muda mfupi baada
ya kutoka uwani kujisaidia.
Newe
amesema
kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mama yake, Thereza Derefa mara
baada ya mumewe kutoka uwani aliingia chumbani na badala ya kurejea
kitandani
alipiga magoti pembezoni mwa kitandani na kuanza kusali huku akitoka
jasho jingi mwilini kiasi cha kulowana na aliamua kumgusa na kumsemesha
ili kujua
kitu gani kilichokuwa kikimsumbua lakini hakujibu kitu.
"Tulimchukua na kumpeleka katika hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, madaktari walimpima ili kuelewa tatizo lakini walibaini
tayari ameishafariki”,amesema Newe.
Tangu Tanzania
ipate uhuru, Jimbo la Shinyanga Mjini limeongozwa na wabunge tisa ambao ni John
Rupia, Bakari Msonde, Anna Tito Kachima, Ntemi Nyanda, Haninghton Mfaume, Paul
Makune, Leonard Derefa, Dk Charles Mlingwa na sasa Stephen Masele.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies