Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MAFUNZO YA UONGOZI WA MAGEREZA DARAJA LA PILI KUFUNGWA 22-JUNE

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Katika jitihada zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kujenga na kudumisha mahusiano baina ya Askari na Maafisa wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, tarehe 22 Juni, 2015 saa 3:00 asubuhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest J. Mangu anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili, katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ambayo yamechukua muda wa miezi minne yalilenga kuwaandaa Maafisa kuwa viongozi wa kati katika vituo vya Magereza nchini. Jumla ya wahitimu ni 216, kati yao Wanaume 161 na Wanawake 44 wanatoka Tanzania Bara, na Wanaume 10 na Mwanamke 10 wanatoka Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.
Sherehe hizo, zitajumuisha mambo yafuatayo:-

* Mgeni Rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
* Mgeni Rasmi kutoa vyeti kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mafunzo ya darasani na
  Mafunzo ya mbinu za medani;
* Mgeni Rasmi kuvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kwa wahitimu wawili kwa niaba
  ya wahitimu wengine na;
* Mgeni Rasmi kutoa Hotuba.
Sherehe za ufungaji wa Mafunzo hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye sherehe hizo siku ya Jumatatu tarehe 22 Juni, 2015 kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Imetolewa na;
                      Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza;
                      Afisa Habari wa Jeshi la Magereza nchini;
                      Makao Makuu ya Jeshi la Magereza;
                      DAR ES SALAAM
                      Juni 19, 2015.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top