Habari za leo ndugu mdau wa Mutalemwa Blog leo nataka nikufahamishe madhara yaliyo tokana na mgomo wa madreva wa daladala jijini Dsm, mgomo huu umedumu takribani siku saba.
Kwa kipindi chote hiki mambo yalikuwa tofauti, maana kwa upande wa wamiriki wa magari yasiyo ya abilia, waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda pamoja na magari madogo ya kubeba mizigo mambo yalikuwa mazuri ususani kwa upande wa mapato yao ya kila siku ukilinganisha na siku za nyuma.
Ndani ya kipindi chote hiki nauri zilipanda mara mbili na zaidi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Ambapo umbali uliokuwa unatozwa Tsh 3,000 kwa madreva wa bodaboda nauri ilipanda mara 2 au 3 kutokana na muonekano wa mtu.
Kwa upande wa magari yasiyo ya abilia pamoja na magari madogo ya kubeba mizigo nauri ilikuwa nikati ya Tsh 1,000 hadi Tsh 3,000 ukilinganisha na siku za nyuma ambapo nauri zilizokuwa zikitozwa na vyombo hivi ni kati ya Tsh 500 hadi Tsh 1,500 tu.
Pia kuisha kwa mgomo huu wa madreva umeacha recod mbaya sana maofisini kwa wafanyakazi wote hapa nchini ususani kwa wafanyakazi wengi wa jijini Dar es salaam.
Maana mbali na wafanyakazi kutozwa nauri kubwa lakini kuchelewa kufika sehemu zao za kazi ni jambo ambalo lilikuwa halipingiki.
Ambapo wale watu walioweza kutembea kwa miguu walionekana kuwai zaidi kuliko wale walio panda magari, japo nawao walikuwa wanafika wakiwa wamechelewa lakini huwezi kuwalinganisha na wale waliopanda magari.
Mwisho kabisa ikiwa ni kushuka kwa uzalishaji wa viwanda na kupungua kwa mapato ya nchi, jambo ambalo linaweza kusababisha uchumi wa nchi kutikisika.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.