Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ISSUE YA MAKASISI KUWADHULUMU WATOTO KIMAPENZI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameonekana kuanza kuwakabili makasisi waliotuhumiwa kwa sakata ya ngono.

Askofu mmoja aliyekua mjumbe wa papa katika jamhuri ya Dominican atafikishwa mahakamani Julai 11. Josef Weslowski raia wa Poland ametuhumiwa kuwaharibu watoto wa kiume pamoja na kuwa na sinema chafu za watoto.

Kwingineko maaskofu wawili wa Marekani wamejiuzulu kwa kukosa kuwalinda watoto ambao walidhulumiwa kimapenzi na makasisi.

Mwanadiplomasia huyo wa zamani,amekuwa katika kifungo cha ndani huko Vatican tangu alipovuliwa wadhfa aliokuwa amepewa na kurudishwa kutoka Jamhuri ya taifa la Dominican mwaka wa 2013.
null

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ameanza kuchukua hatua kali dhidi ya maaskofu wanaowadhulumu watoto. Sasa atakabiliwa na kesi kwa mujibu wa sheria mpya zilizoidhinishwa na Papa Francis.

Hii inamaanisha kuwa anaweza kupewa kifungo cha hadi miaka 12 jela iwapo atapatikana na hatia.

Askofu mwengine wa kanisa la Mtakatifu Paulo huko Minnesota Marekani pamoja na msaidizi wake nao walijiuzulu baada ya kushtakiwa kwamba walishindwa kuchukua hatua dhidi ya kasisi mmoja aliyeripotiwa kumnyanyasa mtoto kingono katika jimbo lake.

Papa Francis na viongozi waliomtangulia wamekuwa wakishtumiwa vikali kwa kukosa kuwachukulia hatua au hata kuwaondoa mamlakani makasisi wanaoripotiwa kwenda kinyume na maadili na hasa unyanyasaji wa kingono.

Pia wamelaumiwa kwa kushindwa kuwawajibisha maaskofu kuongoza makanisa yao kikamilifu. Papa Francis ameidhinisha kamati itakayosikiza na kuadhibu viongozi wa kidini watakaohusika kwa njia yeyote na ukiukaji wa haki za watoto.

Aidha Maaskofu wanastahili kuwachukulia hatua kali makasisi na mapadre waliochini yao wanaoendeleza vitendo hivyo vya dhulma ya kijinsia au hata kutochunguza na kuripoti vitendo kama hivyo kwa polisi.

Mapema mwezi huu Papa Francis aliunda tume maalum iliyopewa mamlaka ya kusikiliza na kuhukumu maaskofu wanaotuhumiwa kufumbia macho vitendo vya unyanyasaji wa kingono ambayo huenda vinaendelea katika makanisa yao.

Kwa namna hiyo , inavyoelekea ni kwamba Papa Francis angependa mashtaka dhidi ya watumishi wa makanisani yashughulikiwe na mahakama maalum ya kanisa badala ya kesi hizo kupelekwa kwa mahakama za kawaida za umma.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top