Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MOTO WA TRA WAWAKIA VIGOGO JUU YA ISHU YA ESCROW

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetua kwa vigogo waliopata mgawo wa fedha za Escrow na kuwataka kulipa kodi ya mapato kwa mujibu wa sheria. Maofisa wa mamlaka hiyo walikwenda kwa vigogo hao na kuwasilisha mahesabu ya kodi walizochukua Januari Mosi mwaka huu 2015 ambapo kila aliyepata mgawo huo ametakiwa kulipa fedha hizo kabla ya Januari 30.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema msimamo wa Serikali unabaki kama ulivyo wa kuhakikisha kila mmoja analipa kodi ya mapato kwa mujibu wa sheria. 

Mwigulu alisema baada ya wahusika hao waliopata mgawo huo wa fedha za Escrow kupelekewa hesabu za kodi, wametakiwa kuhakikisha wanahakiki ndani ya mwezi mmoja na kodi iwe imelipwa. Waliopelekewa hesabu za kodi ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) na aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka waliopata mgawo wa Sh bilioni 1.6 kila mmoja, ambao wanatakiwa kulipa kodi Sh milioni 480 kila mmoja.

Wengine ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), Mbunge mstaafu wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, Jaji Aloysius Mujulizi pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko ambao kila mmoja alipokea Sh milioni 40.4. Hao kila mmoja anatakiwa kulipa kodi ya Sh milioni 12.12.



Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    
In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top