Serikali imesema itatumia askari wa kimataifa wa Interpol kukabiliana na utoroshaji madini ya vito ya Tanzanite nje ya nchi.
Hatua hiyo inakuja huku Kenya na India zikiongoza kwa kuuza Tanzanite kwenye soko la dunia mwaka jana na kuizidi Tanzania ambako ndiko madini hayo hupatikana pekee duniani.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa madini Richard Kasesela alisema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kuchunguza na kubaini njia na mbinu zote zinazotumika kutorosha madini hayo nje ya nchi.
“Kuanzia sasa yoyote atakayekutwa akiuza madini nje ya nchi bila cheti cha uhalisia kinachothibitishwa yametoka Tanzania kupitia njia halali,atakamatwa na kurejeshwa nchini na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi,”alisema Kasesela.
Alisema Serikali haiwezi kuendelea kuvumilia madini na rasilimali zinazopatikana nchini kuendelea kunufaisha watu wa Mataifa mengine.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.