Naibu wa wizara ya fedha bwana Mwigulu Rameck Nchemba amelazimika kutoa ufafanuzi juu ya sarafu mpya ya shilling mia tano, baada ya sarafu hiyo kuzua utata katika maeneo tofauti ndani na nje ya jiji la dar es salaam.
Baada ya wananchi kuikataa sarafu hii wakiwemo madreva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, makondakta wa madaradara nk sasa yatolewa maelezo. A mbapo kiongozi huyu amewatoa hofu wananchi na kuwaomba waendelee kuitumia sarafu hii kwani ni pesa harali ya kitanzania ambayo imeidhinishwa na benki kuu ya Tanzania.
Na akaendelea na ufafanuzi kwakusema kwamba chanzo cha kutengenezwa kwa sarafu hii nikutokana na kuchakaa haraka kwa noti ya shilling 500, ambayo imekuwa ikiingiza gharama kubwa sana katika benki kuu, ambapo katika mzunguko wa noti hiyo imekuwa ikiharibika haraka sana kuliko noti zinginezo jambo ambalo limeonekana kuiingiza benk kuu katika cost zisizo tarajiwa.
kwaiyo basi kutokana na uchunguzi wa kamati ya wizara kubaini tatizo hilo ndipo mchakato wa kuiondoa taratibu noti ya shilling 500 katika system, ambapo kila mzunguzo watakuwa hawatoi noti badara yake watakuwa wakitoa sarafu hii mpya msikilize kiongozi huyu akieleza juu ya sarafu hii bofya hapa.
Pia waziri akamaliza kwa kusema ''badiliko la pesa hii halitoathiri mfumuko wa bei'' kwaiyo watanzania kuweni huru katika kutumia sarafu hii mpya ya Tsh. 500
Mambo yote haya mhe.Mwigulu aliyazungumza jana usiku katika kipindi cha Dakika 45 pale ITV, pia kiongozi huyu aliongelea juu ya watanzania kuwa wazalendo na waungwana katika swalazima la ulipaji wa kodi ya mapato kwa ajiri ya kuiwezesha nchi yetu kuweza kusonga mbele kwa kujiendesha yenyewe bila ya kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi bofya hapa kumsikiliza.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.