Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MGOMO WA WANAJESHI WA IVORY COAST WAPATIWA DAWA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ivory Coast, Hamad Bakayoko ameahidi kuwa Serikali itashughulikia madai ya maelfu ya Wanajeshi walioandamana. Ametoa ahadi hiyo kwa njia ya Televisheni usiku wa jumanne baada ya Wanajeshi kufunga Barabara katika miji muhimu miwili.

Bayoko amesema Wanajeshi hawatawekewa vikwazo vyovyote kutokana na kuandamana kwao. Madai ni ya wanajeshi takriban 9,000 waliokuwa wapiganaji waasi ambao baadae walijiunga na Jeshi.
Wapiganaji hao walikua sehemu ya kikosi kinachomtii Rais Alassane Ouattara aliyechukua madaraka mwaka 2011, na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mapema siku ya jumanne,Waziri wa ulinzi Paul Koffi aliwataka Wanajeshi kurejea kambini baada ya kufunga barabara za mji wa Abidjan na Bouake.
Taarifa za jumatano zinasema Wanajeshi tayari wameondoka mjini Bouake. Haya ni maandamano makubwa kuhusisha jeshi tangu Rais Alassane Ouattara kuchukua madaraka Mji wa Bouake ni ngome ya Rais wa nchi hiyo.
 


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top