Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

EBOLA YASABABISHA NISISHIRIKI FAINALI AMESEMA TRAORE

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mchezaji soka, Ibrahima Traore ameiomba klabu yake ya Ujerumani Borussia Monchengladbach kumruhusu kuichezea timu yake ya taifa ya Guinea katika fainali ya kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2015.
Madaktari wa klabu hiyo wameelezea wasiwasi kuwa huenda akaambukizwa Ebola ikiwa ataenda kuichezea klabu yake nchini Guinea.
Timu ya taifa ya Guinea ,Syli Nationale itacheza katika mechi ambayo lazima washinde dhidi ya Uganda nchini Morocco ambako mechi hiyo ilihamishiwa kwa sababu ya mlipuko wa Ebola nchini Guinea.

''Niliwaambia kwamba ni lazima nichezee klabu yangu,'' alisema Traore. ''Kombe la mataifa ya Afrika ni mchuano muhimu kwa wachezaji wa Afrika kwa hivyo siwezi kukosa fursa ya kucheza katika mechi hizo mbili , zote ni muhimu sana kwangu. ''
''Niliporejea katika klabu yangu nilipimwa na kila kitu kilikuwa shwari, na niliongea na kocha na akasema hapatakuwa na tatizo lolote. Alielewa kama kocha kwamba ni muhimu nisafiri kwenda kuchezea timu yangu, kwa hivyo sina shaka. Sidhani kama kutakuwa na tatizo lolote. ''
Ikiwa Guinea wataicharaza Uganda mjini Casablanca Jumatano, watafuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazochezwa nchini Equatorial Guinea.
Traore anasema kwao kufuzu itakuwa hatua nzuri sana kwa timu hiyo ikizingatiwa matatizo yanayoikabili Guinea wakati huu.
"matatizo yote ambayo tumekuwa nayo, yatatupa nguvu ya kuweza kufanya vyema na ikiwa tutafuzu basi litakuwa jambo jema sana, '' aliseme Traore.
 


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top