Akizungumza na gazeti la grobapublisher wikiendi iliyopita, Hafsa alisema tukio hilo lilijiri hivi karibuni, mishale ya saa 8:00 usiku alipokuwa akitokea Ukumbi wa Delux uliopo Sinza-Kijiweni, Dar akielekea nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama.
“Nilipoangalia nyuma nikaiona pikipiki ambayo nilihisi kama inatufukuzia, lakini kabla sijakaa sawa nikashangaa kumuona Mahamoud ambaye namfahamu kama baunsa na dereva wa bodaboda
“Nilishangaa alipotufikia akiwa na mwenzake kwenye bodaboda alianza kunivuta nje huku Bajaj ikiwa kasi nikapata maumivu kwenye mbavu, michubuko mwilini na kunitegua bega,” alisema Hafsa na kuongeza:
“Baada ya kufanikiwa kuninyang’anya mkoba wangu alitaka kunibaka lakini nilipiga kelele kwa kushirikiana na dereva wa Bajaj niliyopanda ambapo wasamaria wema walijitokeza kunisaidia.
“Alipoona wananchi wamemzingira alitafuta upenyo na kukimbia ndipo nikaenda Kituo cha Polisi cha Urafiki (Dar) ambapo nilipewa fomu namba 3 (PF-3) kwa ajili ya kwenda kutibiwa.
“Nilikwenda kupata matibabu Hospitali ya Palestina (Sinza).
Hafsa Ally akionesha jeraha alilopata ubavuni wakati wa tukio.
“Baada ya kupatiwa matibabu nilimfungulia kesi yenye jalada namba URP/RB/8318/2014- JARIBIO LA UBAKAJI na tayari ametiwa mbaroni,” alisema Hafsa.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.