Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KWELI MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU KADANGANYA UMRI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Kufuatia ushindi alioupata siku ya shindano la kumsaka Miss Tanzania 2014 lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, kuliibuka madai kwamba mrembo huyo alidanganya umri.
MADAI YA JUKWAANI
Awali, akiwa jukwaani kujitambulisha na kujibu maswali, mlimbwende huyo alishika kipaza sauti na kusema:
“My name is Sitti Mtemvu,  ‘am  eighteen years old (jina langu ni Sitti Mtemvu, nina miaka kumi na nane).
Hapo ndipo palipoanzia utata, wanaomjua Sitti walianika umri wake kwamba, ana miaka 25 huku wakianika tarehe ya kuzaliwa kwake kwamba ni Mei 31, 1989. Miandao ikaanza kumponda kwamba alidanganya umri hivyo halimfai tena!
LUNDENGA ATOA TAMKO, ATETEA
Kufuatia hali ya hewa kuchafuka kwenye mitandao, redio na magazeti akishutumiwa Sitti, Oktoba 21, mwaka huu, mratibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliitisha mkutano na vyombo vya habari. Katika mkutano huo ambao Sitti naye alishiriki sanjari na mama yake mzazi, Lundenga alisema vyeti vya kuzaliwa alivyowasilisha mshiriki huyo kama washiriki wengine, vilionesha ana miaka 23, alizaliwa 1991, Temeke jijini Dar.
UTATA WAIBUKA
Utata ulianza kuibukia hapo kwenye maneno ya kutoka kwenye kinywa cha Lundenga kwani alisema cheti hicho kilitolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) Septemba, mwaka huu ikiwa ni siku 32 tu kabla ya shindano la Mlimani City.
MASWALI
Waandishi walitaka kujua hivi; kama cheti hicho kilitolewa Septemba 9, mwaka huu na Sitti amesoma Marekani ambako mtu huwezi kwenda mpaka uwe na paspoti na ili upate paspoti lazima uwe na cheti cha kuzaliwa je, yeye alitumia cheti gani? Maana alikwenda Marekani kati ya mwaka 2010 na 2011.
Sitti alilijibu swali hilo kuwa, cheti hicho kilipotea lakini akashindwa kukitaja kituo chochote cha polisi alichopeleka madai ya kupotelewa kwa cheti na kuishia kusema vyombo vya habari vinamfuatafuata sana.
UFUKUNYUKU WAANZA
Kufuatia mlolongo huo wote, ndipo timu ya uchunguzi ya Magazeti Pendwa ya Global Publishers ikaingia mtaani na kuanza kuchimba ukweli wa umri wa binti huyo. Katika chanzo cha uhakika kutoka katika idara husika ya kutoa paspoti, faili la Sitti lilisomeka hivi: (tunaandika kwa Kiswahili tu).



Jina la ukoo: Mtemvu.
Jina: Sitti Abbas.
Utaifa: Mtanzania.
Tarehe ya kuzaliwa: May 31 1989.
Tarehe ya kutolewa: 17 Feb 2007.
Tarehe ya Mwisho wa matumizi: 14 Feb 2017

Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.

 FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO >>  MUSIC MPYA
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top