Moja kati ya mazoezi ambayo yalifanyika siku ya jana kati ya wanajeshi wa jwtz na jeshi la china.
Wanajeshi wa tanzania wakionesha uwezo wao wakati wa mazoezi ya pamoja
Wanajeshi wa china wakifanya mazoezi kwenye kundi la pamoja na wanajeshi wa tanzania
wanajeshi wa tanzania wakifanya mazoezi
wanajeshi wa china wakionesha uwezo wao kikazi
Baadhi ya viongozi wa serikali ya china wakitazama jinsi vijana wanavyoweza kuonyesha uwezo wao
wanajeshi wa china wakionesha baadhi ya mazoezi kwa wakubwa wao
Wanajeshi wa serikali ya tanzania wakijaribu kuruka kwa njia ya kupiga sarakasi
Moja ya wanajeshi wa china akitandikwa fimbo ya mbavu bila kuumia
mwangalie kijana huyu mwanajeshi wa china kivunja fimbo kwa kuipiga kiwiko kimoja tu
moja kati vijana wa jeshi la tanzania wakionesha uwezo wao wa kuweza kupambana kivita
Kiongozi wa jeshi la tanzania akisalimiana na kiongozi wa jeshi la china
Huyu aliwekewa mikuki miwili shingoni kisha akaanza kujichomachoma lakini hakuweza kutoboka shingo yake wala nini, ni mwanajeshi wa china.
mwanajeshi wa china akivunja vuma kwa njia ya kujipigisha kichwani mwake.
Mwanajeshi wa kikosi maalum cha wanamaji kutoka jeshi la China, akionyesha matumizi ya mikono dhidi ya adui, wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Wanamaji wa China na Tanzania kwenye kamandi kuu ya kikosi cha wanamaji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa JWTZ, Meje Jenerali James Mwakibolwa, (Kulia) na Meja Jenerali Wu Xiao Yi wa jeshi la wanamaji la China, wakibadilishana hati za makubaliano ya mafunzo ya pamoja ya Surpassing 2014
Mazoezi hayo yaliyopewa jina "Surpassing 2014" yalianza kwa maonyesho ya matumizi ya mikono katika kupambana na adui pamoja na maonyesho ya zana za kivita ambapo Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa JWTZ, Meja Jenerali James Mwakibolwa, na Meja Jenerali Wu Xiao Yi kutoka vikosi vya wanamaji vya China, ndio waliozindua mazoezi hayo baada ya kusaini makubaliano ya kufanya hivyo
Askari wa majini wa Tanzania na China, wakiwasubiri maelekezo mwanzoni mwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwenye komandi kuu ya wanamaji wa JWTZ, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO >> MUSIC MPYA