Watu watatu wamekufa na wengine zaidi ya 20 wameokolewa wakiwemo bwana na bibi harusi ambao walitoka kufunga ndoa kufuatia boti waliyokuwa wakisafiria kugonga mwamba na kuzama ndani ya ziwa Tanganyika.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Jafari Mohamed amesema tukio hilo la jana liemtokea katika kijiji cha Kalalangabo wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.
Kamanda Mohamed amesema idadi ya watu haijulikani kwa kuwa mtumbwi ulisafiri nje ya taratibu za kawaida ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya usalama wa nchi kavu na majini (SUMATRA).
Bibi Harusi Mariam Juma akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa kigoma Maweni baada ya kunusurika kwenye ajali ya boti ambayo iligonga mwamba na kuzama kwenye ziwa Tanganyika.
Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa vikosi vya jeshi la wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na wavuvi waliowahi kufika katika eneo hilo walifanikiwa kuokoa watu 20 ambao walikimbizwa hospitali ya mkoa kigoma Maweni kwa matibabu na wengine inawezekana walikimbia ili kupoteza ushahidi wa idadi ya abiria waliokuwa kwenye boti hiyo.
Kwa upande wake Mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa kigoma Maweni, Haika Masula amethibitisha kupokelewa kwa miili mitatu ya watu waliofariki kwenye tukio ambapo mmoja ametambuliwa kwa jina la Salama Juakali huku maiti mbili za watoto zikiwa hazijatambuliwa hadi sasa.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Wavuvi kwenye Mwalo wa kibirizi mjini Kigoma, Sendwe Ibrahimu alisema kuwa katika mahojiano na watu mbalimbali waliokuwa kwenye boti hiyo kumekuwa na takwimu tofauti za idadi kamili ya watu waliopanda boti hiyo huku wengine wakieleza kuwa ni abiria 80, wengine abiria 70 huku baadhi ya ndugu wakieleza kuwa jumla ya watu 40 waliondoka nyumbani kwao Mwandiga kulikofanyika harusi ili kurejea kijijini kwao Mtanga Mwambao wa Kaskazini wa ziwa Tanganyika. Kwa habari kamili bofya hapa.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO >> MUSIC MPYA