Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

BABU WA MIAKA 62 AMBAKA MJUKUU WAKE WIYANI MPANDA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mzee wa miaka 62, Rashid Mbogo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka mitano.

Mtuhumiwa huyo, mkazi wa Kijiji cha Vikonge kilicho katika Kata ya Mpandandogo wilayani Mpanda, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi, Naathaniel Silomba.


Ilidaiwa na mwendesha mashtaka huyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 19, mwaka huu saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake. Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa akiwa anasubiria chakula cha usiku wakati kikiandaliwa na mkewe, alimwita mjukuu huyo na kisha kumpakata mapajani. Alidai kuwa baadaye alivua nguo na kuanza kumbaka huku mtoto huyo akipiga kelele za kuomba msaada kwa kitendo cha babu yake.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa baada ya kusikia mayowe hayo, bibi wa mtoto huyo na majirani waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mtoto sebuleni akiwa anatokwa na damu nyingi sehemu zake za siri huku analia kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo ambayo alikuwa amesomewa na mwendesha mashtaka. Hakimu Chiganga aliieleza mahakama kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi endapo mshtakiwa atatimiza masharti. Mshtakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni. Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo alipelekwa rumande.
  


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top