U.T.I ni maambukuzi katika mfumo wa mkojo ambao hutibika kabisa. Huwa maambukizi haya yanaendelea kuathiri mfumo wako wa mkojo hata pale unapopata tiba sahii au baada ya tiba sahihi huweza kujirudia tena.
Mara nyingi wataalamu wamegundua kuwa UTI Gugu/ inayoji rudia rudia ni pale inapotokea mara mbili ndani ya miezi sita au mara tatu kwa mwaka. Tatizo hili limeonekana kuwa athiri wanawake zaidi kuliko wanaume ikiwa ni kutokana na maumbile kuwa, njia ya haja kubwa kuwa karibu na njia ya haja ndogo na pia uretha zao kuwa fupi kuliko za wanaume. Vyanzo ni maambukiz mapya ya bacteria katika mfumo wa mkojo au ugonjwa kutotibika kabisa pale wanapopewa tiba.
Yapo maambukizi katika kibofu cha mkojo na maambukizi katika njia ya mkojo yani urethra. Maambukizi katika kibofu hutokana na bacteria waitwao Escherichia coli ambao huishi katika utumbo wa binadamu au wanyama ambao husafiri hadi kwenye mfumo wa mkojo pale mtu anapojisafisha kutoka nyuma kwenda mbele baada ya haja kubwa kwa wanawake au pale anaposhiriki ngono kinyume na maumbile na kuhamishiwa uume kutoka njia ya haja kubwa kwenda njia ya haja ndogo.
Pia maji maji yanayoruka kutoka chooni wakati wa kujisafisha ni chanzo. Maambukizi katika njia ya uzazi husababishwa na bacteria waitwao Escherichia coli au pia kwa njia ya magongwa ya ngono kama vile herpes, kisonono au chlamydia. Ni mara chache maambukizi ya ngono kusababisha maambukizi katika kibofu cha mkojo.
DALILI
1. Kukojoa mara kwa mara
2. Mkojo kuwa na rangi nzito ya njano au kuchanganyika na damu
3. Kuhisi kuungua wakati wa kukojoa
4. Maumivu kwenye kibofu, chini mgongoni au chini ya mbavu
5. Kizungu zungu na kutapika
6. Homa
7. Uchovu
USHAURI
Usikiapo au kuhisi dalili tajwa wahi tiba mapema ili kuepukana na madhara zaid.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya
zaidi. FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI