Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KWA NINI MWANAMKE KUTOKWA NA UCHAFU SEHEMU ZA SIRI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Manamke kutokwa na maji maji mepesi na yasiyo na rangi kwenye via vyake vya uzazi ni hali ya kawaida kwani husaidia kuondoa sumu mwilini hasa
baada ya hedhi na wakati wa uzazi.

Lakini ile hali ya mwanamke kutokwa na maji maji yenye rangi tofauti tofauti, mara njano, au rangi kama juisi ya parachichi, na wengine wanakua wanapatwa na miwasho katika via vyao vya uzazi kitaalamu tunaita Abnormal Vaginal Discharge, basi iyo si hali ya kawaida kwa mwanamke na anatakiwa kuchukua hatua juu ya hilo jambo.


Ikumbukwe kwamba mwanamke hawezi kutokwa na uchafu sehemu za siri kama hajatokewa na maambukizi ya aina yoyote yale kwenye kizazi chake, na mwanamke anaepatwa na matatizo kama haya huandamwa sana na hali ya kutokubeba ujauzito au tatizo linalojulikana kama ugumba, na hivo ni vema kulitibia kwa haraka.

DALILI ZAKE NI ZIPI?
Kuna baadhi ya vitu ambavyo mwanamke akiviona basi moja kwa moja ajue kwamba anadalili za ugonjwa huu (Abnormal Vaginal Discharge).

1. Kuwashwa sehemu za uke kwa mwanamke
2. Maeneo ya uke kuwa mekundu kupita kiasi
3. Mwanamke kutokwa na harufu mbaya sehemu za siiri
4. Utokwaji wa uchafu sehemu za siri, kama vile usaha, au maziwa mtindi, au maji maji ya njano au rangi ya kahawia.
5. Maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa,

Kuna maji maji ambayo hutoka sana sehemu za siri za mwanamke, lakini ikumbukwe kwamba maji maji haya yanakua ni ugonjwa pale tu ambapo,

i. Maji maji yanazidi na kutoka kwa kiwango kisicho cha kawaida.
ii. Maji maji yanayotoka kuwa na rangi tofauti kama njano, kahawia, kijani, usaha, au rangi ya maziwa.
iii. Maji maji haya yanapotoka yanaambatana na harufu mbaya sana na kali sana.
iv. Pia maji maji haya yanapotoka yakua yanaambatana na miwasho.

Tatizo hili ni kubwa sana na linawasumbua wanawame wengi sana katika ulimwengu wa sasa, hivyo basi kwa yeyote mwenye kutokewa na baadhi ya mambo kama hayo niliyokwisha kuyataja au mtu wako wakaribu akawa
anapatwa na tatizo kama hili basi ni vema akawasili katka kituo cha afya mapema zaid kwa ushauri na matibabu ya tatizo hilo.

NB. Wanawake najitahidi sana japo kuwaelimisha kwa yale machache ninayoyafahamu kuhusu afya zenu ila muitikio wenu juu ya mambo kama haya ni mdogo sana, kiukweli mpaka mnakatisha tamaa ya mtu kuendelea kutoa elim

=======================================================

Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.

 FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO >>  MUSIC MPYA
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top