Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KUTOKA DODOMA, RAIS KIKWETE NA UKAWA WAUNGA SASA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
KUTOKA DODOMA,RAIS KIKWETE NA UKAWA WAUNGA MKONO KWA USHAURI ULIOTOLEWA NA MTOTO WA MFUGAJI MWIGULU NCHEMBA "SOKOINE WA II" MAPEMA KABLA YA BUNGE LA KATIKA AWAMU YA PILI KUANZA.

Waswahili husema "Dalili ya Mvua ni mawingu" hii ikiashiria wazi kabisa kuwa Naibu Waziri wa Fedha Mh.mwigulu Nchemba anaweza Kuwa Moja ya Viongozi Pekee wenye Mtazamo wa mbali zaidi kwa sasa hapa Nchini hasa kwenye Upande wa Uchumi na Maslahi ya Wanyonge na Masikini.
Hii leo imedhihirika wazi pale Dodoma ambapo Kikao kilichokaliwa na Rais kikwete na Wajumbe wa TCD(UKAWA) kwaajili ya kutafuta maridhiano kuhusu Bunge la Katiba,Hii leo kikao hicho kilichoanza mapema Jana tar.08.09.2014 kimemalizika kwa kuridhia kuwa mchakato Unaoendelea Bungeni hivi sasa utaahirishwa rasmi kwasababu 2/3 haiwezi kupatikana kutokana na UKAWA kuwa nje ya Bunge.

Vile vile Mchakato huo wa Katiba utaendelea Mapema baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.Kwa sasa kutakua na Marekebisho Madogo kwenye Kipengele cha Tume ya Uchaguzi na Mgombea huru awepo.

IKumbukwe mapema Tar.06.08.2014 Mh.mwigulu nchemba alimaarufu Mtoto wa Mfugaji kama wanavyopenda kumuita watanzania alisimama bungeni na kuomba Kiti cha Mwenyekiti wa Bunge kiajiridhishe na uwepo wa 2/3 kwenye Bunge hilo kabla ya kuendele ilikuzuia Matumizi ya Ovyo ya Fedha za Umma endapo 2/3 ingekosekana.

Kauli hiyo ya Mwigulu ilipokelewa Vizuri sana na Watanzania huku baadhi wakisema hii ndio CCM tunayoitaka kwa Viongozi wake kutanguliza Maslahi ya Watanzania na Taifa kwanza.

Baada ya kauli ile,Mwenyekiti wa Bunge la katiba ama aliteleza au alipuuzia ili watu waendelee kunufaika n Posho za Bunge la katiba,Kwa sababu katika hali ya Kawaida tu HOJA YA MWIGULU NCHEMBA YA KUJIRIDHISHA NA UWEPO WA 2/3 ilikuwa na Mantiki sana. Katiba ya sasa inatamuka wazi kuwa Mchakato wa katiba uliopo sasa hauwezi kufanikiwa endapo 2/3 haipo,Kukosekana kwa idadi hiyo ya wajumbe ni dhahiri hata Bunge hili lingekaa miaka 100 katiba isinge patikana kabisa kabisa labda kwa Kuvunja katib.

Hivyo kwa Maana nyingine Mwigulu Nchemba ameuonesha Umma wa Watanzania kuwa kiongozi ni lazima awe na UWEZO WA KUONA MBALI NA KUWEKA MALENGO kw Maslahi ya Umma.

Hatua hii iliyofikiwa na Rais Kikwete hii leo ni dhahiri anamlatia CREDIT mwigulu kuwa ni Kijana aliyekomaa na Mwenyeuwezo wa Kuongoza.Hali kadharika natuma Ujumbe kwa Wajumbe wa Bunge la katiba kuwa Mawazo Muhimu na Komavu kama aliyoyatoa Mwigulu mapema tu wakati Bunge linaanza sio ya kuyapuuzia ni lazima yatendewe kazi.

Mwisho napenda kutoa Rai kwa Watanzania na Wajumbe wote wa Bunge la Katiba,tuungane kuahirisha kwa Mchakato huu rasmi ilikuepusha Utafunaji wa fedha za umma ambazo mwigulu ameapa Kuzitetea kwa hali na Mali iliziwanufaishe watanzania Wa hali ya chini. Hongera RAIS KIKWETE, HONGERA TCD kwa Kuweka Maslahi ya Nchi yetu mbele kwanza.


=======================================================


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.

 FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO >>  MUSIC MPYA
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top