Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

DIAMOND AOKOLEWA NA POLISI BAADA YA KUCHELEWA..

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na mashabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wake katika moja ya maonyesho yake.
Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wake katika moja ya maonyesho yake.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria ambaye pia anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Kwa taarifa zaidi bofya hapa…
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 
          FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top