Taarifa kwa umma: Upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo yote ya ukanda wa Pwani.
Taarifa Namba: 201408-02
Muda wa Kutolewa: Saa 6:00 Mchana
Saa za Afrika Mashariki
Daraja la Taarifa Tahadhali
Kuanzia: Tarehe 01 September, 2014
Mpaka: Tarehe 02 September, 2014
Aina ya Tukio linalotarajiwa:
Hali ya Upepo mkali unaozidi Kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi Mita 2.0 inayotarajiwa katika ukanda wote wa Pwani.
Kiwango cha uhakika: Juu (70%)
Maeneo yatakayo athirika:
Pwani ya mkoa wa Tanga, Dar es salaamu, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Melezo:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya kusini mwa Afrika hivyo kusababisha upepo mkaliwa Kusi,mashariki mwa Pwani ya Tanzania.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada:
Mamlaka ya Hali ya hewa inaendelea kufuatiria hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.
Upatapo taarifa hizi mjulishe na mwenzio tafadhali.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies