Mtandao wa Sony Playstation umefungwa kufuatia shambulizi la mtandao wake wa kutoa huduma ya playstation. Katika ujumbe kwenye mtandao wake , Sony imesema kuwa hakuna habari za watu binafsi zilizohatarishwa kufuatia shambulizi hilo.
Jumapili, ndege aliyokuwa akisafiria mmojawapo wa maafisa wakuu wa Sony, ililazimika kubadilisha mkondo kufuatia hofu ya kulipuliwa. Baadaye ilibainika kuwa kundi linalodai kutekeleza shambulizi hilo la mtandao, kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter uliashiria kuwepo kwa tishio la usalama kwa ndege hiyo.
'Kusuluhisha swala hilo' Katika taarifa hiyo Sony ilisema kuwa “mtandao wa Playstation na mtandao wa burudani wa Sony iliathirika kufuatia jaribio la kufululizia tovuti zao watumiaji wengi na kuizuia kutoa huduma.
"Tutajitahidi kusuluhisha swala hili na tunatumai kuwa tutarejesha huduma zetu haraka iwezekanavyo,” Sony imesema kuwa wapelelezi wa FBI wanachunguza tishio la usalama kwa ndege aliyokuwa akisafiria rais wa Burudani ya Sony Mtandaoni John Smedley, ambayo ilitarajiwa kutua San Diego lakini ikalazimika kubadilisha mkondo na kutua Phoenix, Arizona.
Bwana Smedley alituma ujumbe wa tweeter, "Ndio. Ndege yangu ilibadilisha mkondo. Sitazungumza zaidi ya hayo. Haki itatendeka kwa watu hawa.” Mtandao huo wa sony wenye zaidi ya wateja milioni 52 wa Sony Playstation umewahi kushambuliwa na wavamizi wa mtandaoni hapo awali, likiwemo shambulizi lililoiba habari za siri za mtandao huo, mwaka 2011.
Hii leo Sony inatarajiwa kurekebisha usalama wa mtandao huo ambao hufanyika mara kwa mara kwa mtandao wake wa PlayStation. Baada ya 1740 BST, huduma fulani zikiwemo duka la PlayStation, akaunti ya usimamizi na usajili ya PSN, huduma za burudani na michezo ya mtandaoni hazitakuwepo, kwa sababu ya marekebisho.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI