Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana shutuma zilizoelekezewa kwao kuwa wanahusika na kifo cha aliyekuwamwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Chadema.
Mnyika alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.
Baadhi ya viongozi wa Chadema kutoka kushoto ni Ofisa Habari, Tumaini Makene, Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika, Ofisa Mwandamizi Mafunzo na Uendeshaji, Mohamed Mtoi, na mwenye gwanda ni Katibu Mtendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu, Victor Kimesera.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI