Mkazi mmoja wa kijiji cha Lundusi kata ya Peramiho Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma, bibi Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi maisha ya dhiki na kunyanyaswa sana bila msaadawowote kutoka kwa jamii anayoishi, ali ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza lake alilojiandalia yeye mwenyewe.
Chanzo cha bibi huyu kujichongea jeneza lake nikwamba, alikuwa na hofu yakwamba endapo akifariki dunia je atazikwa kama binadamu wengine? maana jinsi alivyoishi kwa kunyanyaswa hadhani kabisa kama angeweza kupata kuzikwa kama watu wengine wa kawaida.
Bibi Scholastica ni mtu mzima mwenye umli wa miaka 76, napia ni mwenye ulemavu wa viungo anayeishi peke yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi. Pia bibi huyu anasema kuwa ametengwa na jamii yake pamoja na majirani kwa madai ya kwamba eti yeye ni mchawi. Bibi huyu anasema alikuwa na watoto wanne ila wote walifariki dunia wangali bado ni wadogo sana.
Pesa ya kutengenezea ili jeneza nilipata kutoka kwa mfadhili mmoja, wakati mbao nilikuwa nazo nyumbani, kwaiyo kazi ikawa raisi kufanya kazi hii, ila kitendo cha wanajamii pamoja na ndugu zangu kuniita mimi mchawi kinaniuma sana kiukweli (alisema bi Scholastica).
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.