Papa Francis ambaye mwaka mmoja tangu ateuliwa kuwaongoza wakatoliki duniani amekuwa akifanya mabadiliko ya tamaduni na sera za kanisa hilo sasa ametangaza kuwa atambariki askofu Romero licha ya upinzani wa mapapa waliomtanguliwa kutokana na dhana kuwa marehemu Romero alikuwa papa anayewapendelea maskini kinyume na sera za kanisa hilo wakati huo.
Kwa miaka mingi sasa kanisa la katoliki limekuwa likizuia hatua hiyo kwa sababu ya wasiwasi alikuwa na fikra zisizo za kidini. Askofu huyu aliyekuwa mtathmini aliyekuwa amejitokeza wakati wa utawala wa majeshi aliuliwa alipokuwa akisherehekea misa mwaka wa 1980 tarehe 24 mwezi wa machi akiwa mwenye umri wa 62. Kumtangaza mtu mbarikiwa huwa ni kitambulisho muhimu cha kuanza kwa mikakati ya kumfanya kuwa mtakatifu kamili.
Papa alisema siku ya Jumatatu kwamba anatumainia shughuli za haraka za kumbariki askofu huyo. Uchambuzi wa John McManus wa habari za BBC unaeleza kwamba wakatoliki wengi wameshangaa kwa nini mtu ambaye aliuawa kwa kuwatetea maskini amepuuzwa kwa muda mrefu hivo na kanisa ambalo linadai kuwawakilisha maskini.
Matamshi ya papa hayamaanishi kwamba amebadilisha fikra zake juu ya theologia ya ukombozi lakini yanaweza kuwa ya kukiri kwamba kwa wakatoliki wengi Oscar ni mtakatifu tayari kwa vitendo hata kama sio katika jina.
Hakuna mtu ambaye ameshtakiwa kwa mauaji ya askofu huyo na hivyo kutilia pondo dhana kuwa aliuawa na vyombo vya serikali aliyokuwa akiipinga.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI