Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA SOMA ZAIDI HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

JESHI la polisi mkoani hapa limewaua majambazi watatu waliokuwa wamepanga njama ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso  mjini hapa.



Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa,majambazi hao watatu  waliuawa jana tarehe 3 eneo la TBL -Njiro  wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora fedha hizo.

Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba  fedha zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100  huku wakiwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.

Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo  polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika  eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.





Ambapo majibizano yalianza kati ya majambazi hao na polisi huku wakirushiana risasi hadi eneo la TBL njiro ndipo majambazi walipofika eneo hilo waliamua kutelekeza gari na  kushuka chini  na kumimina risasi kwa askari polisi  hao.

Kamanda Sabas alisema kuwa,hatimaye polisi waliweza kuwauawa majambazi hao  na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya  Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.


Aidha Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea kuongeza juhudi hizo zaidi.


Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top