Askofu Gervas Nyaisonga wa jimbo la Katoliki la Mpanda akisalimiana na Mapadri wa jimbo hilo katika eneo la mto koga, ambapo ndipo linapoanzia Jimbo katoliki la Mpanda wakati alipokuwa akiwasili rasmi kwenye jimbo lake jipya la Mpanda akiwa anatokea jimbo la Dodoma.
Askari wa skauti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda wakiwa katika eneo la daraja la mto koga wakimpokea askofu Gervas Nyaisonga alipowasili jana akitokea jimbo la Dodoma ambapo askofu Nyaisonga alipokuwa analiongoza kabla ya kuhamishiwa Jimbo la Mpanda na amesimikwa jana kuwa askofu wa Jimbo la Mpanda.
Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo katoliki la Mpanda akibusu Ardhi hapo jana katika kijiji cha Kamsisi ikiwa ni ishara ya kuhamia rasmi kuliongoza jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma.
Msafara wa waendesha pikipiki wakiwa katika eneo la uwanja wa ndege wa mjini Mpanda wakiwa wanaongoza msafara wa kumpokea askofu Gervas Nyaisonga hapo jana.
Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpanda kabla ya kuanza kwa ibada ya kukabidhiwa ufunguo wa kanisa hilo.
askofu Gervas Nyaisonga ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda ikiwa ni ishara ya kuyaongoza makanisa na kuyasimamia makanisa yote ya jimbo katoliki la Mpanda.
Padri wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Mpanda Padri Matini Kapufi (42 ) pamoja na Katekista wa Kanisa hilo wa Kijiji cha mtakuja Parokia ya Inyonga Katekista Patricki Mwendo wa Saa (60) wamefariki Dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka kwa kuacha njia na watu wengine wawili kujeruhiw na kulazwa hospitalini.
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amesema ajali hiyo ilitokea hapo juzi majira ya saa nne asubuhi katika Kijiji cha Kamsisi tarafa ya Inyonga barabara ya Inyonga kuelekea Mkoani Tabora.
Alisema ajali hiyo ililihusisha gari aina ya Toyota Hilux pick Up lenye namba za usajili T 302 CUY lililokuwa likiendeshwa na Marehemu Padri Martini Kapufi ambaye ni Paroko wa parokia ya Mwese jimbo katoliki la Mpanda.