Leo naomba nianze kwa kuwauliza swali, kwamba wewe jinsi unavyo onekana kwa mtu anaye kutazama, je huo muonekano wako ndio una onesha kipimo cha maisha yako pamoja na tabia zako?
Kwa upande wangu mimi waga nina amini kwamba muonekano wa mtu sio kwamba ndicho kipimo cha tabia zake au kusema kwamba ndicho kipimo cha maisha yake, maana unaweza kukutana na mtu kaulamba kiukweli mpaka ukapagawa, lakini ukimfuatilia kiundani utakuta hayupo kama jinsi anavyo onekana.
Je ndugu msomaji, ivi unafikili ni kwanini watu wengi hawavai uarisia wa tabia zao na maisha yao?