Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amewataka Watanzania kuwa waangalifu ili mchakato wa Katiba Mpya usiwe sababu ya kupigana au kufarakana ili kupata Katiba itakayoendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na ushirikiano.

“Vyovyote mchakato wa Katiba utakavyoishia, tuhakikishe tunabaki na amani na utulivu wetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu, tuhitilafiane bila kupigana,” alisema.
Alisema Watanzania wanapaswa kwa pamoja wasiiharibu nchi yao na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho, vinaendelea kuwaenzi waasisi wa Taifa kwa uadilifu mkubwa.
Akabidhi nyumbaAkikabidhi nyumba hizo, Mkapa alisema ana imani wananchi wanaohudumiwa na zahanati 15 zilizojengewa nyumba hizo wataendelea kufaidika na huduma bora kwa kuwa watumishi wameboreshewa mazingira ya kazi.
Kama mnavyoona nyumba hizi ni za kisasa, zina maeneo muhimu yote yanayokidhi mahitaji ya binadamu, zipo imara na zimekidhi viwango vya ujenzi vinavyostahili,
” alisema. Aliitaka halmashauri zinazohusika kuhakikisha nyumba hizo zinatumika kama ilivyokusudiwa, kutunzwa vizuri na kutengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya ukarabati pale utakapohitajika ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Vijiji vilivyonufaika vipo katika wilaya za Singida Vijijini, Iramba na Manyoni.