Ligi ya mabingwa ya mikoa inatarajia kutimua vumbi leo katika viwanja vitatu tofauti ikijumusisha timu 27 kwa ajili ya michezo ya ufunguzi ikiwa ni kuanza kwa mbio za kusaka nafasi ya timu tatu za kucheza ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa msimu wa mwaka 2014/2015.
Vituo vya ligi hiyo ni pamoja na Morogoro, Mbeya na Shinyanga huku kila kituo kikiwa na jumla ya timu tisa.
Africab Sports ya Tanga itafungua dimba dhidi ya Kiluvya katika mchezo utaofanyika saa 8 mchana wakati saa 10 jioni Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma itayochuana na Pachoto ya Mtwara ikiwa ni michezo ya ufunguzi kwa kituo cha Morogoro kwenye jamhuri.
Simiyu United FC ya Siminyu itaonyeshana kazi na Mvuvumwa FC ya Kigoma ikipigwa majira ya saa 8 mchana na Wenda FC ya Mwanza ikiteremka dimba saa 10 jioni kucheza na Eleven Stars FC ya Kagera michezo ikichezwa katika kiwanja cha Kambarage.
Kituo cha Morogoro kina timu za African Sports ya Tanga, Kilivya United FC ya Pwani, Mji Mkuu ya Dodoma, Pachoto SC ya Newala Mtwara, Bulyanhulu FC ya Shinyanga, Kariakoo FC ya Lindi, Navy FC ya Dar es Salaam, Abajalo FC ya Dar es Salaam na Mshikamano FC ya Dar es Salaam.
Kwa kituo cha Mbeya ina timu za Ujenzi FC ya Rukwa, Volcan FC ya Morogoro, Arusha FC ya Arusha, Panone FC ya Kilimanjaro, Mpanda United ya Katavi, Magereza FC ya Iringa, Tanzanite FC ya Manyara, Njombe Mji FC ya Njombe na Town Small Boys ya Ruvuma.
Kwa upande wa kituo cha Shinyanga inajumuisha timu za Simiyu United ya Simiyu, Mvuvumwa FC ya Kigoma, Wenda FC ya Mwanza, Eleven Stars FC ya Kagera, Singida United ya Singida, Mbao FC ya Mbeya, JKT Rwankoma ya Mara, Geita Veterans ya Geita na Milambo FC ya Tabora.
Mshindi wa kwanza wa kila kundi atafuzu kucheza ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI